Ajira Wizara Ya Afya 2022. The Ministry of Health has approved 1650 jobs for cadre specialists various Health Services who will be employed and assigned to work centers which are under the direct operation of the Ministry of Health.

This is a fulfillment of the promise made by the Sixth Phase Government headed by Mr. Samia Suluhu Hassan, President of the Republic
of the Union of Tanzania.

Approval of those 1650 vacancies from the Office of the President – SERVICE provides opportunities for professionals of various cadres in delivery centers services under direct operation to the Ministry of Health.

TAARIFA KWA UMMA
SERIKALI YATOA KIBALI CHA AJIRA ZA WATUMISHI 1650 KWA
VITUO VYA KUTOA HUDUMA ZA AFYA CHINI YA UENDESHAJI WA
MOJA KWA MOJA WA WIZARA YA AFYA

Dodoma, Jumamosi Aprili 16, 2022.

Wizara ya Afya imepata kibali cha ajira 1650 za Wataalamu wa kada
mbalimbali za Afya ambao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi
ambavyo vipo chini ya uendeshaji wa moja kwa moja wa Wizara ya Afya.
Huu ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Kibali cha nafasi hizo za ajira 1650 kutoka Ofisi ya Rais – UTUMISHI
kinatoa fursa kwa wataalamu wa kada mbalimbali katika vituo vya kutoa
huduma chini ya uendeshaji wa moja kwa moja kwa Wizara ya Afya
Aidha, kada ambazo zitanufaika na nafasi hizi ni pamoja na; Madaktari
Bingwa (25), Madaktari (215), Wafamasia(15), Maafisa Maabara(62),
Wateknolojia (Dawa, Maabara, Mionzi, Macho-155), Maafisa Uuguzi (140),
Maafisa Uuguzi Wasaidizi (467), Wauguzi (140), Wakemia (2), Madaktari
wa Afya Kinywa na Meno (15), Tabibu Meno (19), Watoa Tiba kwa Vitendo
(15), Wazoeza Viungo kwa Vitendo(31), Maafisa Wazoeza Viungo (33),
Maafisa Afya Mazingira(40), Wasaidizi wa Afya (134), Wahandisi Vifaa
Tiba (17), Wateknolojia Vifaa Tiba (40) na Watunza Kumbukumbu wa Afya
(10) na Madereva (4).

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

i. Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo
yenye upungufu mkubwa wa wataalam wa Kada za Afya, na
hakutakuwa na kubadilisha kituo cha kazi ndani ya miaka
mitatu(3). Maeneo hayo ni kama ifuatavyo; Hospitali za Rufaa za
Mikoa; (1) Kigoma; (2) Katavi; (3) Sumbawanga; (4) Songwe; (5)
Njombe; (6) Ruvuma; (7) Mtwara; (8) Lindi ; (9) Simiyu; (10) Geita;
(11) Shinyanga; (12) Tabora; (13) Singida; (14) Manyara; na (15)
Mara; Hospitali za Kanda, Chato na Mtwara, Hospitali ya Magonjwa
Ambukizi Kibong’oto pamoja na Vyuo vya Afya. Hivyo, waombaji
wawe tayari kupangiwa katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu.
ii. Waombaji ambao hawatakuwa tayari kwenda kwenye maeneo tajwa
hapo juu inashauriwa kutotuma maombi.
iii. Waliopo masomoni hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi za ajira.
iv. Mwombaji atapaswa kuchagua maeneo matatu ambayo angependa
kupangiwa kazi endapo atachaguliwa.
v. Mwombaji mwenye nia ya kwenda kufundisha katika Vyuo vya Afya
aainishe wakati wa kutuma maombi kwenye mfumo pamoja na barua
ya maombi.
Ajira hizo zinategemewa kwenda kupunguza uhaba wa watumishi
kutokana na Serikali kujenga Hospitali mpya pamoja na kuendeleza
Miundombinu ya utoaji wa Huduma za Afya.
Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa
Tangazo hili (kuanzia tarehe 16/04/2022). Maombi yote yawasilishwe kupitia
mfumo wa ajira wa Wizara ya Afya unaopatikana kupitia tovuti: ajira.moh.go.tz.
*Muombaji atakayeomba kupitia ya Wizara ya Afya, ASIOMBE kwa nafasi hiyo
hiyo kwa upande wa OR-TAMISEMI.

Imetolewa na:
Prof Abel N. Makubi
KATIBU MKUU WIZARA YA AF

Please follow and like us: